Wednesday 6 April 2016

ASKARI 500 WA MAREKANI WALIJIUA 2015…!!

Takaribani askari 500 wa Jeshi la Marekani walijiua mwaka jana, na hivyo kuendeleza mkondo wa
idadi kubwa ya wanajeshi wanaojiua nchini humo katika kipindi cha miaka saba iliyopita.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon katika ripoti yake ya Ijumaa ilisema kuwa, askari 265 walio katika vikosi vya anga, bahari, nchi kavu na kikosi cha marine walijiua mwaka 2015.

Aidha askari 210 wa ziada katika jeshi la Marekani walijiua mwaka jana.

Mwaka 2001 wanajeshi 145 walijiua katika Jeshi la Marekani na idadi hiyo imekuwa ikiongezeka kila mwaka.


Msemaji wa Pentagon Luteni Kanali Hermes Gabrielle, amesema kuzuia vitendo vya wanajeshi kujiua ni suala linalopewa kipaumbele na Jeshi la Marekani.

0 comments:

Post a Comment