Wednesday 13 April 2016

WAFUGAJI WAPIGWA STOP KWENDA NA SILAHA ZA JADI KWENYE MIKUSANYIKO…

Watu wa jamii ya wafugaji wamepigwa marufuku, kwenda na silaha za jadi katika sherehe mbalimbali hasa za harusi.

Amri hiyo imetolewa na uongozi wa serikali ya kijiji cha Ntatumbila wilayani Nkasi Rukwa, kutokana na silaha hizo kuhatarisha usalama.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Ignas Kanjele, amepiga marufuku hiyo katika mkutano wa kijiji uliofanyika jana.
Amesema katika kijiji hicho kumekuwa na tabia ya muda mrefu kwa wafugaji kutembea wakimwa na sime, mikuki, mapanga na marungu, hali inayosababisha hofu kwa baadhi ya wananchi kwa kuwa hawajui usalama wao.

Mwenyekiti huyo wa ulinzi na usalama wa kijiji hicho, amesema kutokana na watu hao kutembea na silaha, baadhi yao wamekuwa wakiwapiga wananchi na hata kuwajeruhi, hali ambayo amesema haivumiliki kijijini hapo.

0 comments:

Post a Comment