Wednesday 27 April 2016

ALIYEVUMBUA PLEASE CALL ME ASHINDA KESI…!!

Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika Kusini, imeiamuru kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kumlipa mwanamume aliyebuni wazo la kutuma ujumbe wa kuomba apigiwe simu.

Gazeti la Sowetan la Afrika Kusini linasema kuwa mwajiriwa wa zamani wa Vodacom Nkosana Makate, aliiambia mahakama kwamba huduma ya "please call me" ilitokana na wazo lake.
Huduma hiyo humuwezesha anayetumia simu kutuma ujumbe bila malipo kwa wateja wengine akiwaomba wampigie simu.
Tovuti ya Tech Central ya Afrika Kusini inasema kuwa, haijabainika Bw Makate atalipwa shilingi ngapi na Vodacom.

Lakini awali amewahi kuambia Moneyweb kwamba uvumbuzi wake huo,ulizalishia ampuni hiyo karibu randi bilioni 70 za Afrika Kusini na alitaka alipwe 15% ya pesa hizo.

0 comments:

Post a Comment