Katika mataifa mengi ya Afrika wakati wa uchaguzi, wanasiasa hutoa pesa
ili kuwashawishi wapigaji kura kuwachagua.
Lakini amini usiamini huko
Korea Kusini, polisi wameanzisha uchunguzi baada ya kuibuka madai kuwa wapiga
kura wenye umri wa makamo, walimpigia mwanasiasa fulani kura eti kwa sababu
aliwapa vidonge vya kuongeza nguvu za kiume!
Mbunge wa eneo la Suwon
iliyoko karibu na mji mkuu wa Seoul, ndiye anayetuhumiwa kwa njama hiyo.
Jimbo la Suwon ilishuhudia
upinzani mkali,katika uchaguzi uliofanyika Jumatano iliyopita.
Hata hivyo jina la mshukiwa mkuu, halijatajwa hadi pale
ushahidi utakapopatikana.
Lakini uchunguzi wa msingi
umethibitisha kuwa, mgombea huyo alikuwa na kiwango kikubwa cha madawa ya kuongeza
nguvu za kiume kwa wakati mmoja.
Haijabainika ni kwa nini wala
alikusudia kuwapa kina nani, na chunguzi bado unaendelea.
0 comments:
Post a Comment