Friday 12 February 2016

SERIKALI YAAPA KUPAMBANA NA WANAOUZA UNGA…!!

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Charles kitwanga, amesema atapambana wauzaji
wa dawa za kulevya, bila kujali ukubwa wa mtu ambaye anajihusisha na boasahara hiyo haramu.
Akizungumza wakati wa kupokea vifaa vya kurahisisha kazi kwa jeshi la polisi kutoka ubalozi wa marekani mkoani Arusha, kitwanga amesema vita dhidi ya dawa ya kulevya inapaswa kuungwa mkono na viongozi wa jeshi hilo katika mikoa yote ya Tanzania.
Michael Soylim kutoka ubalozi wa marekani amesema kuwa,vifaa hivyo vinagharimu zaidi ya dola elfu 4 za Marekani, na kusema ubalozi huo utaendelea kusaidia nchi ya Tanzania katika kuimarisha ulinzi na usalama haswa kwa jeshi la polisi.
Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoan Arusha Liberates Sabas, amesema vifaa hivyo walivyopokea ni vya kisasa, ambavyo vitawezesha kukabiliaana na matukion ya uhalifu.

Vifaa vilivyokabidhiwa pamoja na jeshi la polisi mkoani Arusaha ni pamoja na Aadio call 27 na magari tisa ya kufanyia doria ili kupambana na wahalifu.
Bonyeza play hapo chini kumsikia Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Charles kitwanga,akieleza zaidi.

0 comments:

Post a Comment