Tuesday 16 February 2016

MBUNGE ZIMBABWE AVUNJA REKODI YA BUSU AFRIKA…!!

Mbunge mmoja nchini Zimbabwe Joseph Chinotimba, ameingia katika kumbukumbu
za Afrika baada ya kumbusu mke wake Vimbai kwa muda mrefu zaidi kuwahi kurekodiwa barani Afrika.
Mbunge huyo na mkewe walizoa tuzo hiyo baada ya kupigana busu kwa dakika 10 na sekunde 17.
Rekodi hiyo iliwekwa katika hafla moja iliyopigiwa upatu na kunadiwa kuwa Mashindano ya busu refu zaidi kuwahi kutokea barani Afrika.
Hafla hiyo ilipangwa na kuandaliwa kwa ushirikiano na waandalizi wa Daftari la rekodi barani Afrika.

Hafla hiyo iliandaliwa katika mji mkuu wa Harare, kama sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao iliyoadhimishwa jumapili.

0 comments:

Post a Comment