Wednesday 17 February 2016

AJABU YA MWANAMKE KUSHIKA MIMBA JELA VIETNAM..!!

Askari jela 4 nchini Vietnam wamesimamishwa kazi kwa kosa la kuzembea kazini, baada ya
mfungwa wa kike aliyehukumiwa kunyongwa kushika mimba.
Wachunguzi wanasema mfungwa huyo mwenye miaka 42, alijitungisha mimba kwa kutumia mbegu za kiume kutoka kwa mfungwa wa kiume ili kukwepa hukumu ya kifo.
Sheria ya Vietnam inasema mwanamke mjamzito au mwenye mtoto wa chini ya umri wa miaka mitatu, hawezi kunyongwa na badala yake hukumu yake inafaa kubadilishwa na kuwa kifungo cha maisha jela.
Sasa inatarajiwa kwamba hukumu yake itapunguzwa kutoka kifo hadi maisha jela, kwa sababu atakuwa na mtoto wa chini ya miaka mitatu.
Maafisa wanasema mwana mama huyo alinunua mbegu kutoka kwa mfungwa wa kiume mwenye umri wa miaka 27 kwa kati ya dollar elfu 2 na 300 na paundi elfu 1 na 600.

Mfungwa huyo alimpa mwana mama huyo mbegu zake mara mbili Agosti mwaka 2015,na mwanamke huyo anatarajiwa kujifungua mwezi Aprili.

0 comments:

Post a Comment