Thursday, 11 February 2016

AJALI YAUA 11 TANGA, YAJERUHI 29..!


Watu 11 wamefariki dunia leo huku wengine 29 wamejeruhiwa, baada ya Basi la Simba Mtoto
kugongana uso kwa uso na lori katika kijiji cha Pangamlima wiliyani Muheza.
Kamanda wa polisi Mkoani Tanga Mihayo Msikhela, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa Basi la Simba Mtoto lilikuwa linatokea Tanga kuelekea jijini Dar es salaam.
Kamanda Mihayo ameeleza kuwa ajali hiyo imetokea mapema leo, baada ya dereva wa lori kusinzia wakati akiendesha gari hilo na kuhama njia na kukutana uso kwa uso na basi hilo.
Pia kamanda Mihayo amesema kati ya watu 11 waliopoteza maisha ni pomoja na madereva wa magari hayo yote mawili.
Kamanda Mihayo ameongeza kuwa majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Muheza, huku jitihada zikifanyika kuwapeleka abiria watano ambao hali zao ni mbaya katika hospitali ya rufaa ya KCMC mkoani Kilimanjaro.
Bonyeza kitufe cha play hapo chini kumsikia kamanda Mihayo akitoa taarifa ya Ajali hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment