Mauaji ya watu waliohukumia kifo kiholela nchini Saudi Arabia, yameongezeka
katika mwaka huu wa 2016.
Gazeti la al Rayul Aam limeripoti kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2016
hadi sasa zaidi ya watu 63 wameua kwa kukatwa vichwa nchini Saudi Arabia, suala
linaloakisi mwenendo wa kupanda juu takwimu za kuuliwa watu nchini humo.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi Arabia, ilitangaza jana kuwa imewanyonga
watu wawili mmoja wao akiwa raia wa Yemen.
Katika mwaka uliopita Saudi Arabia iliwanyonga au kuwaua kwa kuwakata vichwa
watu 153, idadi ambayo ilikuwa kubwa zaidi ya mwaka wa kabla yake kwa asilimia
80.
Saudi Arabia inakosolewa sana na jumuiya za kimataifa na taasisi za kutetea
haki za binadamu, kwa kutekeleza hukumu za vifo kiholela dhidi ya wapinzani wa
utawala wa kifalme wa nchi hiyo, na watetezi na wanaharakati wa kupigania haki
za kijamii.
0 comments:
Post a Comment