Hatimaye
walimu katika jijini Dar es Salaam nchini Tanzania wataanza kusafiri bure bila
ya kutozwa nauli.
Hatua hiyo ambayo itawahusu
walimu wa shule za serikali, imechukuliwa katika juhudi za kutafutia ufumbuzi
matatizo ya walimu kutokana na mshahara wanaolipwa kuwa mdogo na usiokidhi
mahitaji.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul
Makonda ameutangaza uamuzi huo wa walimu kusafiri bure wanapoelekea na kurudi
kazini, baada ya ombi alilolitoa kuwaombea walimu walioko katika wilaya yake,
kwa wamiliki wa mabasi hayo ya usafiri maarufu kama daladala, kukubaliwa.
Uamuzi huo utaanza kutekelezwa
kuanzia Machi saba, lakini muda wao wa kusafiri bure utaanzia saa kumi na moja
na nusu alfajiri hadi saa mbili alfajiri na kuanzia saa tisa hadi saa kumi na
moja jioni,na kwamba zaidi ya muda huo watalipa nauli.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Chama cha Madereva mkoa wa Dar es Salaam Shabani Mdemu, amesema wamekubali
kuwabeba walimu bure, lakini kwa shartu wasipande wengi katika basi moja.
0 comments:
Post a Comment