Wanasayansi nchini Marekani
wametengeneza roboti inayofanana na mende,
ambayo inaweza kutumiwa kuwaokoa
watu kunapotokea tetemeko la ardhi.
Watafiti
wanasema roboti hiyo inatumia mbinu zinazotumiwa na mende, kutembea kwenye
nyufa kupenya vifusi na kuwaokoa walionaswa katika maporomoko.
Wanasayansi
hao wanasema kuwa endapo roboti hiyo inawezavishwa kamera kisha ikatumwa kwenye
vifusi vya jengo lililoporomoka,inaweza kurahisisha uchunguzi wa usalama wa
vifusi kabla ya makundi waokoaji kuingia.
Ukubwa
wa roboti hiyo ni sawa na kiganja cha mwanadamu.
Roboti hiyo inaweza
kupenyeza katika mianya midogo maradufu ama nusu wa ukubwa wake.
Miguu
yake inapanuka kama vile mende.
Utafiti
huo umechapishwa katika jarida la kisayansi lijulikanalo kama ''Proceedings of
the National Academy of Sciences''.
0 comments:
Post a Comment