Tuesday 2 February 2016

WAJAWAZITO KUKOSA OLIMPIKI BRAZIL..!!

Wanawake wajawazito wameshauriwa kutosafiri kwenda Brazil kushuhudia mashindano ya Olimpiki mwaka 2016 kwa sababu ya hatari ya virusi vya Zika.

Serikali ya Brazil imesema kuwa hawashauri wanawake wajawazito kwenda kwenye michezo ya Olimpiki jijini Rio De Jeneiro mwezi Agosti

Hatua hii imekuja punde baada ya shirika la afya duniani WHO kutangaza hali ya dharura kutokana na madhara yatokanayo na virusi vya Zika.

0 comments:

Post a Comment