Tuesday 23 February 2016

SOKWE AZALIWA KWA UPASUAJI..!!

Mwana wa Sokwe anaendelea vyema, baada ya kuzaliwa kupitia upasuaji katika hali isiyo ya kawaida.

Sokwe huyo alizaliwa kupitia upasuaji usio wa kawaida,baada ya mamaake kuonyesha ishara za ugonjwa hatari wa shinikizo la damu.
Alihitaji msaada wa kupumua lakini sasa madaktari wanasema hali ya mama na mtoto iko shwari.
Kumekuwa na sokwe wachache waliofanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua duniani, kisa cha hivi majuzi kikiwa kile cha San Diego Safari Park mwaka 2014.

Sokwe huyo aliye na siku 11 alizalishwa na Professa David Cahill, ambaye amewazalisha wanawake wengi kupitia upasuaji,lakini ilikuwa mara yake ya kwanza kumzalisha sokwe.

0 comments:

Post a Comment