Wednesday 24 February 2016

NDEGE ILIYOWABEBA WATU 21 YATOWEKA NEPAL….

Ndege ndogo iliyowabeba abiria 21, imetoweka ikiwa maeneo yenye milima nchini Nepal.

Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Pokhara magharibi mwa mji mkuu Kathmandu, kwenda Jomsom eneo ambalo watu wengi wanaoenda kukwea milima ya Himalaya huanza safari yao ya kukwea milima hiyo.
Hakuna viwanja vya ndege kati ya maeneo hayo mawili na inahofiwa kwamba ndege hiyo imeanguka.

Ndege hiyo ni ya shirika la ndege la Tara Airlines.

0 comments:

Post a Comment