Wednesday, 10 February 2016

UTAFITI: FARASI HUBAINI HISIA ZA MWANADAMU..!

Farasi huweza kubaini kati ya mtu aliye na furaha na aliye kasirika, kwa kuangalia uso wa mwanadumu utafiti umesema.

Katika jaribio kwa kutumia picha za mwanamume wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Sussex, walionyesha kwamba farasi wanaofugwa nyumbani huchukizwa na sura zilizokasirika.
Wanasayansi hao wanasema kuwa ufugaji huo, huenda umewawezesha farasi kuelewa tabia za binaadamu.
Matokeo hayo yamechapishwa katika jarida la Biology Letters.
Kundi hilo lilifanya vipimo vyake kwa kuwasilisha picha nyingi mbele ya farasi 28.
Matokeo yake alielezea ni kwamba waliangalia picha za watu waliokasirika na jicho lao la kushoto.
Akili za wanyama zimeumbwa kana kwamba hisia zinazotolewa na jicho la kushoto, huangaziwa na eneo la kulia la ubongo ambalo hutumiwa kuangazia hisia mbaya.
Watafiti hao pia waliweka vipimo vya moyo katika moyo wa farasi hao, ambavyo vilibaini kwamba nyuso zilizokasirika hufanya moyo wa wanyama husika kudunda kwa haraka.

Matokeo kama hayo yameripotiwa miongoni mwa mbwa, na kuzua maswali kuhusu ni vipi kuishi na binaadamu kuna badili tabia za wanyama hao.

0 comments:

Post a Comment