Usafirishaji wa silaha duniani
umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni, huku Marekani ikiendelea
kuongoza
katika biashara ya silaha na Urusi ikiwa ya pili.
Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti mpya
wa taasisi ya kimataifa ya amani mjini Stockholm nchini Sweden SIPRI, silaha
zilizosafirishwa barani Afrika, Asia na Mashariki ya Kati zimeongezeka.
Ripoti hiyo inasema kiwango cha
silaha kubwa zilizosafirishwa, kilikuwa asilimia 14 zaidi katika kipindi cha
kati ya mwaka 2011 na 2015, ikilinganishwa na miaka mitano kabla, huku Marekani
na Urusi zikisafirisha silaha nyingi.
Nchi zilizoagiza silaha nyingi ni
India, Saudi Arabia, China na Falme za Kiarabu.
Watayarishaji wa ripoti hiyo
waliuzungumzia mzozo wa Yemen wakisema muungano wa nchi za kiarabu unaopambana
na waasi wa Houthi nchini humo, unatumia silaha nzito za kisasa kutoka Marekani
na Ulaya.
0 comments:
Post a Comment