Friday, 5 February 2016

MGODI WAPOROMOKA AFRIKA KUSINI…

Takriban wachimba mgodi 52 wamekwama ardhini, ndani ya mgodi wa dhahabu mashariki mwa Afrika Kusini kulingana na chombo cha habari cha News24.

Kisa hicho kilitokea mwendo wa saa mbili asubuhi,kulingana na daktari mmoja wa kutoa matibabu ya dharura Jacques Ainslie.
Mojawapo ya shimo liliporomoka na kuwanasa wachimba mgodi 52.
Kufikia sasa asilimia 70 ya wachimba mgodi hao ama wafanyikazi 30 wameokolewa,bwana Ainslie alikiambia chombo cha habari cha News24.
Wachimba mgodi waliojeruhiwa wamesafirishwa katika hospitali moja kwa matibabu.
Hatahivyo watu watatu bado hawajulikani waliko, na bwana Anslie amesema anashuku huenda wamekwama katika chumba ambapo mporomoko huo ulianza.


Related Posts:

  • UNAWEZA KUSAFIRI UKITUMIA NDEGE ISIYO NA RUBANI....? Hilo ndilo swali mamilioni ya watu huenda wakajiuliza siku za usoni ikiwa wanataka kusafiri kwenda likizo kote duniani. Tunaposogea karibu na kutumia magari yasiyokuwa na dereva, ambayo tayari yameingia barabarani katika… Read More
  • FACEBOOK KUJA NA RUNINGA YA MTANDAONI.. Kampuni kubwa zaidi ya mitandao ya kijamii duniani Facebook, inatarajia kuanza kutoa huduma ya video itakayokuwa ikiitwa ”watch” ama tazama. Facebook inasema kwamba imewekeza mamilioni ya dola katika kuufanya mfumo hu… Read More
  • KIPINDUPINDU CHAANZA KUSAMBAA MBEYA.......... Wakati ugonjwa wa kipindupindu ukiendelea kuwatesa wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani hapa, ugonjwa huo umepiga hodi ndani ya jiji la Mbeya na hadi leo Alhamisi wagonjwa watano waligundulika. Meya wa jiji hilo, Mchu… Read More
  • MKAPA MIONGONI MWA WAATHIRIWA WA UPANUZI WA BARABARA... Nyumba inayoaminika kumilikiwa na mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Tanzania Benjamini Mkapa itavunjwa ili kuruhusu upanuzi wa barabara ya Morogoro. Nyumba hiuyo ya Anne Mkapa itakuwa miongoni mwa maelfu ya nyumba, a… Read More
  • VIDEO MPYA:ROMA ASIMULIA ALIVYOTEKWA…. Rapa Roma Mkatoliki ameachia video ya wimbo wake ‘Zimbabwe’ ukiwa ni wimbo wake wa kwanza tangu alipotekwa na kuteswa kwa siku tatu. Kupitia ‘Zimbabwe’ Roma amesimulia tukio la utekaji wake,  watu anaoamini walimt… Read More

0 comments:

Post a Comment