Friday, 12 February 2016

MTOTO ALIYEZALIWA MOYO UKIWA NJE AFARIKI…!!

Mtoto aliyezaliwa katika hospitali ya wilaya ya Meru mkoani Arusha akiwa na tatizo la moyo kuwa
nje amefariki dunia.
Mganga mkuu wa wilaya Meru Dr Ukio Boniface, amesema mtoto huyo alizaliwa tarehe tisa na tatizo hilo,na madaktari walijitahidi kuokoa uhai wake lakini ikashindikana.
Hata hivyo Dokta Ukio ameitaka jamii kutolihusisha jambo hilo na imani za kishirikiana, na badala yake waweze kusikiliza ushauri na utaalamu unaotolewa na madaktari.
Bonyeza play hapo chini kumsikia Dr Ukio akielezea zaidi tukio hilo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment