Tetemeko kubwa la ardhi limekumba
Taiwan Kusini, na kuangusha jengo moja la ghorofa 17 ambapo hadi kufikia sasa
watu watatu wamethibitishwa kufariki.
Tetemeko
hilo la kipimo cha Ritcher 6.4 lilitokea karibu na mji wa Tainan.
Zaidi
ya watu 200 wameokolewa kutoka kwa jengo hilo, ingawa waokoaji wangali
wanajaribu kuwafikia watu wengine ambao inadhaniwa wangali wamekwama katika
mabaki ya jengo hilo.
Tetemeko
hilo liligonga usiku wa manane wakati watu wengi walikuwa wamelala.
Kumetokea
matetemeko mengine madogo matano mda mfupi baada ya tetemeko hilo kuu.
Idara
ya kusimamia maswala ya chini ya radhi inasema kuwa tetemeko hilo lilitokea
sehemu ya juu pekee, hali ambayo husababisha madhara makubwa zaidi.
0 comments:
Post a Comment