Saturday, 6 February 2016

TZ YAPAMBANA KUTOKOMEZA UKEKETAJI........

Tarehe Sita Februari ni siku ya kutokomeza aina zote za ukeketaji watoto wa kike na wanawake duniani.

Umoja wa Mataifa ulifikia uamuzi huo kwa kuzingatia kuwa kitendo hicho pamoja na kukiuka haki za binadamu, kinakwamisha harakati za maendeleo ya kundi hilo wakati huu ambapo dunia inasaka siyo tu ulinzi wa kila binadamu bali pia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.
Nchini Tanzania Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la idadi ya watu linashirikiana na wadau kutokomeza mila hiyo potofu.
Miongoni mwa wadau ni Children’s Dignity Forum,ambao Kiwale11 blog ilimuuliza kurugenzi mtendaji wake Koshuma Mtengeti sasa wamefanya nini.

Bonyeza Play hapo chini kumsikia Koshuma akieleza zaidi walipofanikiwa.

0 comments:

Post a Comment