Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amefunga bao
lake la kwanza
Ulaya wakati timu yake Genk ikichapa Club Brugge kwa mabao 3-2
katika Ligi Kuu Ubelgiji.
Samatta aliyeingia akitokea benchi
katika dakika 77, alitumia dakika nne tu kupachika bao lake la kwanza na
kuihakikishia timu yake pointi tatu muhimu kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa
Cristal Arena. Hicho ni kipigo cha kwanza kwa vinara wa Ligi Kuu Ubelgiji, Club
Brugge mwaka huu.
Club Brugge ilianza mchezo kwa kasi
na kufanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia Thomas Meunier, lakini Genk
iliamka na kupata bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika 36 mfungaji
akiwa na Nikolaos Karelis, kabla ya Thomas Buffel kuongeza la pili dakika ya
50.
Samatta alipachika bao la tatu kwa
wenyeji katika dakika ya 81, Club Brugge ilipata bao la pili kupitia Hans
Vanaken katika dakika 83.
Hata hivyo, siku hiyo nzuri ya
Samatta iliingia doa baada ya kuonyeshwa kadi njano katika dakika ya 90.
0 comments:
Post a Comment