Thursday, 9 June 2016

HII NDIYO MIKOA INAYOONGOZA KWA UTAPIA MLO NCHINI..!!


Pamoja na maendeleo yaliyotokana na kukua kwa pato la wastani la Mtanzania na kupungua kwa
umasikini wa mahitaji ya msingi, serikali imeainisha mikoa mitano iliyokithiri kwa umasikini wa kipato.
Akiwasilisha bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi ya 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016/17, Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango, amesema mkoa unaoongoza ni Kigoma ambao wakazi wake asilimia 48.9, wanakabiliwa na umasikini uliokithiri wa kipato.
Mikoa mingine yenye umasikini wa kipato ni Geita (asilimia 43), Kagera (asilimia 39), Singida (asilimia 38.2) na Mwanza (asilimia 35.3).
Katika wilaya zilizokithiri kwa umasikini wa kipato, ni Kakonko mkoani Kigoma na Biharamulo mkoani Kagera, ambapo Dk Mpango amesema katika wilaya hizo, takribani asilimia 60 ya watu wake, wako chini ya mstari wa umasikini wa mahitaji ya msingi.
Tathmini ya hali ya umasikini kimaendeleo iliyoainisha umasikini huo, imetumia takwimu za Sensa ya Watu ya mwaka 2012 na Utafiti wa Hali ya Kipato na Matumizi katika Kaya wa 2012, ulionesha pia ahueni ya umasikini katika mikoa mitano.
Dk Mpango ametaja mikoa hiyo yenye ahueni na idadi ya watu wanaokabiliwa na umasikini wa kipato katika mabano kuwa ni Dar es Salaam (asilimia 5.2), Kilimanjaro (asilimia 14.3), Arusha (asilimia 14.7), Pwani (asilimia 14.7) na Manyara (asilimia 18.3).
Pamoja na tathmini ya kimkoa na kiwilaya lakini katika nchi nzima, amesema kati ya mwaka 2010 na 2015, Pato la Mtanzania liliongezeka kutoka Sh 770,464.3 kwa mwaka mpaka Sh milioni 1.9 mwaka 2015 sawa na mara 2.5.

Related Posts:

  • BIASHARA YA UKAHABA YAPIGWA STOP UFARANSA.! Bunge la Ufaransa limeidhinisha sheria mpya, inayopinga biashara ngono nchini humo. Hatua hiyo inadaiwa kwamba huenda ikaathiri maisha ya watu zaidi ya elfu thelathini, ambao wanategemea shughuli za ngono katika kujipat… Read More
  • VIROBA VYAPIGWA MARUFUKU ARUSHA..! Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda, amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi aina ya kiroba katika mkoa wake. Amesema uamuzi huo unatokana na vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa, kushindwa kufanya kazi na kulewa wakati … Read More
  • ASKARI 500 WA MAREKANI WALIJIUA 2015…!! Takaribani askari 500 wa Jeshi la Marekani walijiua mwaka jana, na hivyo kuendeleza mkondo wa idadi kubwa ya wanajeshi wanaojiua nchini humo katika kipindi cha miaka saba iliyopita. Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentag… Read More
  • LEO NI KUMBUKUMBU YA KIFO CHA AMANI ABEID KARUME… Leo April 7, 2016 ni siku ya kumbukumbu ya miaka 44 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ambaye alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi. Mzee Karume al… Read More
  • IRAN, PAKISTAN NA SAUDIA ZINAONGOZA KWA KUNYONGA….. Shirika la haki za kibibaadamu la Amnesty International limesema kuwa, kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu walionyongwa ulimwenguni mwaka uliopita, ikilinganishwa na kipindi chochote tangu mwaka 1989. Takriban w… Read More

0 comments:

Post a Comment