Wednesday 29 June 2016

PADRI APIGA MARUFUKU LIPSTICK KWA MAHARUSI….!


Waumini wanawake wanaokwenda kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Hananasif
Kinondoni jijini Dar es Salaam, wamepigwa marufuku kupaka rangi ya mdomo Lipstick’ wakati wa ibada ya misa takatifu ya ndoa.
Rangi hiyo ya mdomo ni moja ya vipodozi ambavyo hutumiwa na wanawake kwa ajili ya urembo, kwa lengo la kunogesha mwonekano wake na kuvutia mbele za watu.
Uamuzi huo ulitangazwa juzi jioni na Paroko wa Parokia ya Hananasif Kinondoni jijini Dar es Salaam Padri Gasper Mtengeti, wakati wa ibada ya misa ya kumwombea marehemu Rose Michael iliyofanyika kanisani hapo.
Kutokana na hali hiyo Pandri Mtengeti amewataka wanawake kuacha kupaka rangi wakati wa misa takatifu, ambapo alitoa sababu tatu zinazotokana na Liturijia ya Ekaristi Takatifu (utaratibu wa uendeshaji wa ibada) chini ya Kanisa Katoliki.
Pandri Mtengeti ameeleza sababu hizo kuwakataza maharusi wa kike kujipaka rangi ya mdomo, ambapo amesema rangi hiyo inayopakwa huwa inasalia katika chombo kinachobeba divai ambayo kiimani kwa dhehebu hilo ni Damu ya Yesu Kristu.
Sababu ya pili ni kwamba rangi ya mdomo huwa inachanganyika na damu ya Yesu wakati wanapokunywa, kitendo ambacho si chema mbele za Mungu.

Na sababu ya tatu rangi hizo hubaki kwenye kitambaa cheupe, kinachotumika kufuta kikombe cha hostia baada ya kuguswa na midomo ya mtu mara baada ya kunywa.

0 comments:

Post a Comment