Tuesday 7 June 2016

WACHINA WAONGOZA KUINGIA TZ KINYUME CHA SHERIA.!

Raia wa China wameelezwa kuongoza kuingia nchini kinyume cha sheria, katika kipindi cha
miezi minne (Januari mpaka Aprili) wakifuatiwa na Waethiopia.

Naibu Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka Wilson Bambaganya, ametoa taarifa hiyo jana katika mkutano na wanahabari akisema jumla ya wahamiaji haramu elfu 4 mia 7 na 92 wamekamatwa nchini katika kipindi hicho.
Amesema changamoto kubwa katika udhibiti wa wahamiaji haramu ni ukubwa, na uwazi wa mipaka yetu sanjari na uwanda mkubwa wa bahari.

Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Utawala na Fedha ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Abbas Irovya, amesema operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu nchini imefanikisha kubaini waliokamtwa.

0 comments:

Post a Comment