Friday, 24 June 2016

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA AJIUZULU….!

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika muungano wa Ulaya.

Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo angatuke.
Bw Cameron ambaye ameongoza kampeini ya kusalia katika muungano wa EU amesema kauli hiyo imempa mshutuko mkubwa na kwa baadhi ya watu mashuhuri duniani.
Akiongea katika kikao cha waandishi wa habari nje ya afisi yake jijini London, Bwana Cameron amesema kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofanywa.
Sauti yake iliibua hisia hasa aliposena naipenda saana taifa hili na najihisi vizuri kuliongoza muda huo wote.
Bwana Cameron amesema kuwa kauli ya wengi sharti isikizwe japo hafahamu kwanini Waingereza walichukua uamuzi kama huo ilhali taifa hilo lilikuwa linaufanisi mkubwa sana ndani ya EU.

Cameron akiwa ameandamana na mkewe amesema bila shaka sasa utawala mpya unahitajika utakaoweza kutathmini mbinu na mkataba wa kujiondoa kutoka kwa muungano huo wa bara Ulaya.

Related Posts:

  • MILIPUKO YATOKEA UWANJA WA NDEGE BRUSSELS… Moshi umeonekana ukitoka kwenye moja ya majumba katika uwanja huo Milipuko miwili imetokea katika uwanja wa ndege wa Zaventem mjini Brussels.Moshi umeonekana ukitanda angani kutoka kwa moja ya majengo katika uwanja huo. … Read More
  • HUYU NI PAKA MWIZI WA NGUO ZA NDANI ZA WANAUME…!! Paka mmoja mwizi wakati wa usiku, amekuwa akiiba soksi pamoja na nguo za ndani nchini New Zealand. Katika kipindi cha miezi miwili paka huyo mwenye umri wa miaka sita kwa jina Brigit kutoka mji wa Hamilton, aliiba bukta… Read More
  • DR SHEIN ATANGAZWA MSHINDI WA URAIS ZANZIBAR… Uchaguzi wa marudio Zanzibar jana, ulifanyika katika hali ya utulivu tofauti na baadhi ya watu walivyokuwa wakifikiria. Hali ya amani na utulivu ilitanda kuliko uchaguzi wowote uliofanyika tangu kuanza kwa mfumo wa … Read More
  • HII HAPA NGOMA MPYA YA SUGU:FREEDOM Msanii Nguli wa mziki wa HIP HOP hapa nchini ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA Joseph Mbilinyi,ameachia wimbo wake mpya unaitwa FREEDOM baada ya kukaa kimya kwa kipindi kirefu. Wimbo huo umefan… Read More
  • HOSPITALI ZATUMIA MAJI YENYE VINYESI… Utafiti uliofanywa umebaini kuwa asilimia 46.5 ya hospitali hapa nchini, zinatumia maji yenye vimelea vya kinyesi (Ecoli). Kauli hiyo ilitolewa juzi jijini Dar es Salaam na mtafiti ambaye pia ni mtaalamu wa mazin… Read More

0 comments:

Post a Comment