Friday 24 June 2016

ALIMWA KADI NYEKUNDU KWA KUPUMUA MBELE YA MWAMUZI….!

Mchezaji wa Sweden ameonyeshwa kadi nyekundu baada ya mwamuzi kumtuhumu kuwa alifanya vitendo visivyokuwa vya ‘kiungwana’ na ‘kiuanamichezo’ uwanjani.

Adam Lindin Ljungkvist anayeichezea Pershagens SK, alikuwa uwanjani katika mchezo dhidi ya kikosi cha akiba cha Jarna SK kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Saba Sweden.
Hata hivyo beki huyo wa kushoto alionyeshwa kadi ya pili ya njano iliyomtoa uwanjani dakika ya 93, baada ya kupumua akiwa karibu na mwamuzi.
“Nilikuwa na mchafuko wa tumbo, hivyo nikajikuta nimeshaponyokwa,” alisema nyota huyo wa miaka 25 alipozungumza na Lanstidningen Sodertalje.
“Nilimuuliza mwamuzi, ‘hivi, siruhusiwi kupumua hata nikiwa nimebanwa?’ ‘Hapana,’ alinijibu…
Sikuelewa, lakini labda alidhani nilifanya hivyo mkononi na kumrushia puani. Lakini sikufanya hivyo.”


 “Nilizungumza na mwamuzi na nikamwambia sikufanya makusudi bali ilikuwa  ni  mchafuko wa tumbo.”

0 comments:

Post a Comment