Thursday, 23 June 2016

BABA AJIWEKA TATOO KUFANANA NA MWANAWE ALIYEFANYIWA UPASUAJI…

Baba wa miaka 28 nchini Marekani amenyoa kichwa chake na kuweka mchoro wa tattoo, unaofanana na kovu la kichwa cha mwanawe aliyefanyiwa upasuaji.

Josh Marshall ambaye anatoka Kansas aliingia katika shindano la kila mwaka, linaloendeshwa na shirika la hisani kuhusu saratani ya watoto na kushinda taji la #BestbaldDad {baba mwenye kipara kizuri} wikendi iliopita.
Akikiri aliandika: Mimi na mwanangu katika hafla ya St. Baldtricks huko Wichita Kansas.
Niliwekwa tatoo ya kovu la mwanangu ili kuimarisha motisha yake.
Shindano hilo huwashirkisha watu wa familia na marafiki wa mtoto aliye na saratani.
Mwanawe alipatikana na uvimbe katika ubongo mnamo mwezi Machi.

''Mwanangu alikuwa na wasiwasi mwingi baada ya kufanyiwa upasuaji,alijihisi kama hayawani'',alisema Josh Marshal.

Related Posts:

  • Daktari ampiga ngumi mgonjwa na kumuua..!! Kanda ya video ya CCTV, imetolewa ambapo daktari mmoja nchini Urusi alimpiga ngumi mgonjwa na kumuua. Kisa hicho kilitokea katika mji wa Belgorod kilomita 670 kusini mwa mji mkuu wa Moscow, mnamo mwezi Disemba tarehe 29 … Read More
  • Homa ya Lassa yauwa 35 Nigeria.! Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Nigeria kutokana na ugonjwa wa homa ya Virusi vya Lassa, imeongezeka mpaka 35 kutoka watu 2 jana. Mikoa iliyoathirika na kutoa wagonjwa wengi zaidi ni pamoja na Ibadan Oyo, Taraba, … Read More
  • Perfume inaweza kukuletea balaa..!! Kama wewe ni kati wale ambao wanakwepa kuoga wakitegemea mtelezo wa Perfume,sikiliza hiii stori tokea huko nchini  Uingereza. Ni kwamba kijana mmoja Thomas Townsend mwenye umri wa miaka 16, amefariki d… Read More
  • Kitabu kipya cha Papa kuchapishwa…. Makao makuu ya kanisa katoliki mjini Vatican yamefichua maelezo kuhusu kitabu kipya cha papa Francis "the name of God is Mercy" jina la Mungu ni rehema, kitakachochapishwa kote duniani kwa muda wa siku mbili zijazo. Maan… Read More
  • Wavaa vimini wacharazwa bakora..!! Viongozi wa Kitongoji cha Kasalazi kilichoko katika Kijiji cha Kanyara wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, wanadaiwa kuwachapa fimbo hadharani wanawake wanaovaa nguo fupi na za kubana zinazoonyesha baadhi ya sehemu zao za … Read More

0 comments:

Post a Comment