Wednesday 8 June 2016

KESHI AFARIKI DUNIA….

Nahodha na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi (54) amefariki
dunia mapema leo jijini Benin katika jimbo la Edo State.
Msiba huu umekuja ikiwa ni mwaka mmoja umepita tangu mwanasoka huyo ampoteze mkewe, Kate Keshi, baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.
Keshi atakumbukwa kuwa miongoni mwa wanasoka wa kipekee kabisa nchini Nigeria kwani amewahi kutwaa kombe la Mataifa ya Afrika akiwa mchezaji na kama kocha wa kikosi cha Super Eagle.
“Keshi hakuwa mgonjwa kabisa, hajawahi kuonyesha dalili zozote za ugonjwa, lakini tunahisi kifo kimesababishwa na msongo wa mawazo mara baada ya kifo cha mkewe,” mmoja wa marafiki wa Keshi ameliambia TheCable.


Keshi alizaliwa Januari 23, 1962 huko Azare katika jimbo la Bauchi na kuanzia soka lake katika timu ya ACB Football Club, baadaye akajiunga na klabu za New Nigeria Bank, Stade d’Abidjan, Africa Sports, Lokeren, Anderlecht na RC Strasbourg.

0 comments:

Post a Comment