Wednesday 22 June 2016

SHEREHE YA KULA NYAMA YA MBWA YAANZA CHINA…!

Sherehe ya kila mwaka ya kula mbwa imeanza jana kusini mwa taifa la China licha ya pingamizi kutoka katika taifa hilo na ugenini

Takriban mbwa Elfu 10 na paka kadhaa wanatarajiwa kuuawa na kuliwa, wakati wa sherehe hiyo ya siku kumi inayofanyika Yulin.
Wanaharakati wanasema kuwa hafla hiyo ina ukatili huku wale wanaotaka sherehe hiyo kupigwa marufuku wakiandikisha saini milioni 11.
Mamlaka ya eneo hilo inasema kuwa sherehe hiyo haiungwi mkono moja kwa moja na serikali lakini hufanywa na wafanyibiashara wa kibinafsi.
Sherehe hiyo ya mlo wa nyama ya mbwa huwaleta pamoja watu wengi, katika eneo la Yulin ili kujichagulia nyama ya mbwa, matunda na vinywaji.


Utamaduni wa kula nyama ya mbwa ulianza miaka 500 iliopita nchini China, Korea Kusini pamoja na mataifa mengine, ambapo wengi wanaamini mlo huo huondoa joto mwilini wakati wa majira ya kiangazi.

0 comments:

Post a Comment