Tanzania ni
miongoni mwa mataifa chache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini
mengi.
Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu,
sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi
adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa
ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway, wamegundua uwepo wa takriban
futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.
Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la
Tanzania.
Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao
wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki
haswa kwa madaktari, ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za
utabibu zijulikanazo kama MRI scanners.
Kabla ugunduzi
huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa
2035.
Mnamo mwaka wa
2010 Mwanfisikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson, alikuwa ametabiri
kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.
Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu kuhimiza kutungwa
kwa sheria, itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama
vile kwenye vibofu, kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi
kuliko ile ya Oxygen.
Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford amesema kuwa, Gesi
iliyoipata Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za
mashine za MRI.
0 comments:
Post a Comment