Muungano
wa sekta ya filamu za ngono nchini Japan umeomba msamaha na kuahidi kuifanyia
mabadiliko sekta hiyo kufuatia madai kwamba wanawake wanalazimishwa kufanya
ngono katika filamu.
Muungano wa kunadi picha hizo
umesema kuwa unaomba msamaha kwa kushindwa kujichukulia hatua .
Hatua hiyo inajiri baada kundi la
wanaharakati kuwaonya wanawake ambao wanateswa katika sekta hiyo.
Sekta hiyo ya filamu za ngono
nchini Japan imekuwa ikikashifiwa kwa unyanyasaji wa haki za kibinaadamu.
Lakini shaka kuhusu mfumo wa
sheria unawafanya waathiriwa kushindwa kujitoa na kulalamikia tatizo hilo.
Mnamo mwezi Machi,shirika moja la
haki za kibinaadamu,lenye makao yake mjini Tokyo lilisema kuwa linajua kuhusu
ongezeko la visa ambavyo wanawake walio na matumaini ya kuwa wanamitindo
wanalazimishwa kujihusisha katika kanda za video zilizo chafu.
0 comments:
Post a Comment