Friday, 10 June 2016

MTOTO WA NYANI’ ADAIWA KUBAKA MWANAFUNZI…!

Kijana Baraka Joshua (23) inayedaiwa alikuwa akiishi na nyani baada ya kuzaliwa na
kutupwa porini mkoani Shinyanga takriban miaka minane iliyopita, amepandishwa kizimbani Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kujibu mashtaka ya kumbaka na kumlawiti mtoto wa miaka tisa.
Alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Florida Wenceslaus. Alidai Mei 17 eneo la Shule ya Msingi Tabata Kimanga,mshtakiwa alitenda makosa hayo dhidi ya mtoto ambaye alikuwa anasoma katika shule hiyo.
Mshtakiwa huyo alikana mashtaka na kurudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Hakimu Catherine Kiyoja aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 26, ikapotajwa tena.

Awali mshtakiwa anadaiwa alikuwa anaishi na nyani kabla hajachukuliwa na askari wa wanyamapori baada ya kumfuatilia kwa karibu.

Related Posts:

  • MAELFU WAANDAMANA NORTH CAROLINA…. Maelfu ya waandamanaji wamesafirishwa kwa mabasi hadi katika mji mkuu wa jimbo la North Carolina nchini Marekani ili kufanya maandamano. Waandamanaji hao wameenda ili kuunga mkono na wengine kupinga sheria mpya ya kit… Read More
  • UKILALA KATIKA KITANDA KIPYA HUTALALA VYEMA…!! Je ushawahi kugundua kuwa ukilala katika kitanda au mazingira mapya haupati usingizi wa kutosha? Sasa Utafiti umebaini kuwa mtu akilala katika mazingira mapya ubongo wake haulali wote! Upande wa kushoto wa ubongo huw… Read More
  • KICHAA CHA MBWA HUU WATU ZAIDI YA 1000 KILA MWAKA NCHINI…. Imeelezwa kuwa watu elfu 1 mia 6 hasa watoto hufa nchini kila mwaka, kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa. Hayo yalielezwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Mary Mashingo. Dk Mashingo … Read More
  • WAKATI BORA WA KUPEWA CHANJO YA HOMA… Na utafiti nchini Uingereza unaonesha kuwa, chanjo ya homa ni bora zaidi iwapo mtu atapewa majira ya asubuhi badala ya alasiri. Watafiti wamebaini kuwa uwezo wa mwili wa mtu una nguvu mno kuwa na matoke bora iwapo mtu a… Read More
  • MKE WA KIBAKI AFARIKI…… Mke wa Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki Lucy Kibaki, amefariki dunia leo jijini London, Uingereza alipokuwa akipatiwa matibabu. Kwa mujibu wa taarifa ya Rais Uhuru Kenyatta, Lucy Kibaki amefariki katika hospitali ya … Read More

0 comments:

Post a Comment