Bajeti ya Serikali iliyotangazwa huenda ikapunguza idadi ya watu
wanaopenda kuonekana
tofauti, kwenye usajili wa magari kwa kuandika majina yao
badala ya namba.
Wamiliki wa magari wanaotaka kusajili
namba binafsi kama kuweka majina yao, sasa watalipa Sh10 milioni badala Sh5
milioni za awali, kwa kipindi cha miaka mitatu.
Akitoa mapendekezo ya mapato na
matumizi ya Serikali kwa mwaka 2016/17 jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk
Philip Mpango aliomba Bunge liridhie kufanya marekebisho ya Sheria ya Magari
(Kodi na uhamisho wa umiliki) ili kupandisha usajili wa namba hizo.
Namba hizo binafsi zilizoanzishwa
miaka minne iliyopita, zinaruhusu mtumiaji kuandika jina au neno lolote kwenye
gari lake tofauti na namba za kawaida zinazotumika nchini.
0 comments:
Post a Comment