Friday 10 June 2016

ZITTO ASEMA ALICHOHOJIWA NA POLISI…!!

Jeshi la polisi kanda maalumu ya dar es salaamu lilimuita na kumuhoji mbunge wa kigoma mjini
Zitto Kabwe, kwa ajili ya kupata ufafanuzi juu ya maudhui ya hotuba aliyo itoa jumapili iliopita katika viwanja vya Zakhiemu Mbagala.
Mheshimiwa Kabwe alifika katika ofisi ya polisi kanda maalumu ya Dar es salaamu,ambapo alihojiwa kwa masaa mawili.
Baada ya hapo mheshimiwa Kabwe alizungumza na waandishi wa habari, ambapo alionesha kusikitishwa na uamuzi huo huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatiwa kwa haki ya mkusanyiko kwa wananchi.

Kiwale 11 blog imepiga story na Zitto Kabwe,na amefunguka kile ambacho amehojiwa na jeshi hilo la polisi, ponyeza play hapo chini kumsikiliza.

0 comments:

Post a Comment