Wednesday 8 June 2016

HILLARY CLINTON AWEKA HISTORIA MAREKANI…!

Vyombo vya habari vya Marekani vilibashiri Clinton atakuwa na wajumbe wa kutosha kuwa chaguo
la Democratic, katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba.

Pia vyombo hivyo vya habari vya Marekani vilisema Clinton tayari ana wajumbe elfu 2 mia 3 na 83, wanaomuunga mkono ambao aliwahitaji ili kupata uteuzi wa chama.
Hii inajumuisha wajumbe wakuu ambao wapo huru, kumuunga mkono mgombea yeyote lakini tayari wameahidi kumuunga mkono Clinton.
Mgombea mtarajiwa wa urais kwa chama cha Republican Donald Trump, amemshambulia vikali anayeonekana mpinzani wake kutoka chama cha Democratic Hillary Clinton siku ya Jumanne, akimshutumu kwa kuuza fursa kwa wizara ya mambo ya nje ya Marekani wakati alipokuwa waziri wa mambo ya nje.
Trump alitoa maneno makali alisema Clinton na mume wake Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton wamegeuza siasa kujinufaisha binafsi.

Trump alizungumza katika usiku ambao Hillary Clinton, ameweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kupata uteuzi usio rasmi wa chama ili kuwania urais, baada ya uchaguzi wa awali katika majimbo sita uliofanyika siku ya Jumanne.

0 comments:

Post a Comment