Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), imekamata tani laki
sita za tende mpakani
mwa Kenya na Tanzania, eneo la Hororo zilipokuwa
zikiingizwa nchini kwa ajili ya kuanza kuuzwa.
Mkurugenzi wa TFDA Thomas Nkoro
amesema: “Tumezikamata tende hizi kwakuwa hazina taarifa ya iana yoyote kwa
mlaji na zilikuwa zimefungashwa katika vifungashio visivyo faa.”
Amesema zilikuwa zimehifadhiwa kwenye
magunia na madumu ya bati ambayo si rafiki kwa afya ya binadamu.
Hata hivyo, amesema Tende hizo zinasadikika kuwa tayri zilishapata
kutu kutokana na vifungashio vyake na tayari baadhi ya watu waliokula tende
hizo wameanza kulalamika kuumwa tumbo.
0 comments:
Post a Comment