Friday 10 June 2016

WANASAYANSI WAGEUZA HEWA YA SUMU KUWA JIWE…!!

Watafiti wanaoendesha uchunguzi katika eneo la Ice land, wanaamini kuwa wanaweza kupunguza
hewa chafu inayochafua mazingira kwa kunasa hewa ya sumu ya carbon dioxide, na kuigeuza kuwa mawe.
Wanasayansi hao waliyeyusha hewa hiyo ndani ya maji,kwa kupuliza mchanganyiko wake ardhini ambako ilichanganyika na madini ya volcano, na kuunda mawe yanayofanana na chokaa.
Wanasayansi hao wamesema mfumo huo unaweza kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya viwango vya joto duniani, kwa sababu mawe ya volcano inayohitajika kugeuza gesi hiyo yanapatikana kote duniani.
Utafiti huo wa miaka miwili uligharimu takriban dola milioni 10.
Wanapendekeza kuwa hiyo itakuwa njia dhabiti ya kupambana na tabia nchi japo itagharimu pesa nyingi.
Mradi huo unaotambuliwa kama CarbFix, unaweza kunasa hewa ya sumu kutoka angani na kuipenyeza kupitia kwenye mabomba na maji hadi ardhini.
Shughuli hiyo inakamilika kwa asilimia 95% ya hewa hiyo kuganda na kuwa jiwe.


0 comments:

Post a Comment