Thursday 30 June 2016

SIAFU WAUA BWANA HARUSI…!!

Wakazi  wa Kijiji  cha  Nditu,  Kata  ya Suma, Wilaya ya Rungwe  mkoani Mbeya, wamegoma
  kuzika mwili wa marehemu Shabani  Yusufu (27),  baada kushambuliwa na kundi la  siafu nyumbani kwake  na kusababisha apoteze uhai.

Yusufu amefariki dunia ikiwa ni siku moja tu baada ya kufunga ndoa na kuzua gumzo kubwa kijijini hapo, jambo ambalo linahusishwa na imani za kishirikina.
Akisimulia mkasa huo baba mzazi wa marehemu Ebron Mwaipaja, amesema mwanawe alitoka kufunga ndoa juzi na alikutwa na mauti hayo akiwa amejipumzisha chini ya mti nyumbani kwake, ambako ghafla alivamiwa na siafu.
Amesema kulikuwa na maneno ya hapa na pale wakati wa maandalizi ya harusi hiyo kutoka kwa baadhi ya watu, ambayo yamesababisha tukio hilo kuhusishwa na imani za kishirikina.
Baba huyo amesema baada ya tukio hilo, wananchi na uongozi wa Serikali ya kijiji walifika eneo hilo, huku wakimtaja mmoja wa wanakijiji kuwa ndiye aliyetuma siafu hao.
Amesema wananchi waligoma kuandaa taratibu za mazishi wakishinikiza aletwe mganga wa jadi apige ramli, ili kumbaini mtu anayeendesha matukio ya ushirikina yanayoendelea kijijini hapo.

Ameeleza kuwa baada ya wananchi kugoma kuzika serikali ya kijiji nayo iligoma kutoa kibali ili mganga aitwe, ikisema siku zote Serikali haiamini uchawi, jambo ambalo lilisababisha wananchi waliokuwa na silaha za jadi, kufanya maandamano na kufunga barabara.

0 comments:

Post a Comment