Soko la panya waliogunduliwa na Chuo Kikuu cha Kilimo
cha Sokoine (SUA) wenye uwezo wa kutegua
mabomu na kubaini ugonjwa wa kifua
kikuu, limezidi kuongezeka baada ya nchi nyingi kuwahitaji.
Nchi za Cambodia, Vietnam,
Thailand na nyinginezo zilizopitia katika vita, zimeonesha kufanikiwa na panya
hao, na sasa wanahitaji wengine zaidi ya 10 ili kusambaza katika maeneo
mbalimbali ya nchi hizo.
Pia nchini Ethiopia wamehitaji
panya zaidi ya 10 kwa ajili ya kubaini ugonjwa wa kifua kikuu, kutokana na
panya hao kuwa na uwezo wa kubaini mgonjwa ambaye ugonjwa huo haujaonekana kwa
vipimo vya kawaida.
Mtafiti wa Kituo cha Utafiti
na Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu wa SUA Dk Georgies Mgode,amesema awali
panya wa kutegua mabomu waliishapelekwa katika nchi za Msumbiji, Angola na 16
Cambodia na kuonesha mafanikio makubwa sana.
Amesema kwa sasa wanaomba
vibali katika Wizara ya Maliasili na Utalii kupeleka panya hao wanaohitajika,
katika mwisho wa mwaka huu au mwanzoni mwa mwakani.
0 comments:
Post a Comment