Chuo Kikuu
cha Kilimo cha Sokoine (SUA), kimepata suluhisho la kupunguza kuzaliana panya
nchini kwa
kuanzisha uzazi wa mpango kwa wanyama hao.
Akizungumza
na waandishi jijini Dar es Salaam Mtaalamu wa Kilimo wa Chuo hicho Thoneson
Mhamphi, amesema utafiti huo ambao upo katika hatua za awali haujaweza
kusambazwa.
Mhamphi
amesema dawa hizo za uzazi wa mpango zinazojulikana kama Quinestro na
Levonorgester, zimekuwa zikichanganywa kwenye chakula na kuwapatia panya hao
hatua itayowafanya washindwe kuzaliana.
Amesema utafiti
huo unaendelea kufanyika katika hatua nyingine, kuona jinsi ya kukabiliana na
panya waliopo mashambani.
Msikilizaji
kama hukuwa ukifaamu ni kwamba, panya wana kasi ya kuzaliana na anaweza kuzaa
kila baada ya wiki tatu.
Vilevile
panya ana uwezo wa kupata mimba tena saa 24 baada ya kuzaa.
0 comments:
Post a Comment