Ripoti
ya mwaka 2016 ya Uchumi wa Simu za Mikononi Afrika inasema kuwa,
Tanzania ni
miongoni mwa nchi nane Afrika zenye soko kubwa la simu za mikononi.
Ripoti
hiyo iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana kwenye mkutano wa wanne wa mwaka
wa Chama cha Kampuni za Simu (GSMA Mobile 360 Afrika), inatokana na utafiti
uliofanywa na GSMA Afrika.
Ripoti
hiyo inasema Tanzania inaungana na nchi za Nigeria na Ethiopia ambazo kwa utatu
wao, ndio zinazochukua zaidi ya theluthi moja ya soko simu ya mikononi barani
Afrika.
Ripoti
hiyo imebainisha kuwa zaidi ya watu nusu bilioni Afrika wamejiunga na huduma ya
simu za mkononi, na wengi wao wakijiunga na huduma na intaneti inayopatikana
kwenye simu zao.
0 comments:
Post a Comment