Tuesday 12 July 2016

MUSEVENI ASIMAMISHA MSAFARA WAKE KUPOKEA SIMU…!!

Rais wa Uganda bwana Yoweri Kaguta Museveni, amezua kihoja katika kijiji kimoja karibu na
mpaka wa Uganda na Tanzania aliposimamisha msafara wake wa magari iliapokee simu faraghani.
Amini usiamini Rais Yoweri Museveni ameshuka kutoka kwenye gari lake rasmi, akachukua kiti chake na kukiweka kando kando ya barabara mpya ya Isingiro ikipitia kijiji hicho cha Kyeirumba hadi Tanzania, na kupokea simu faraghani.
Mzee Museveni kama vile baba wa taifa, alitumia muda wake kufanya shughuli hiyo huku akiwapungia mkoo wapita njia.
Baada ya dakika 30 hivi raia wa kijiji hicho walishangaa kuwa miongoni mwa maafisa wakuu serikalini.
Ilikuwa ajabu sana kwao kumuoana Museveni akiwa ameketi barabarani.
Waganda katika mitandao ya kijamii wamesambaza picha hiyo ya rais museveni akizungumza kwa simu ambayo inaonekana kuwa sio ya kisasa.

Wengine wanamkejeli kwa kuhofia kudukuliwa huku wengine wakimdharau kwa kitendo hicho.

0 comments:

Post a Comment