Mwaka
huu wa 2016 huenda ukawa ndio wenye joto kali zaidi kuwahi kurekodiwa, kufuatia
hali ya joto
duniani kuweka rekodi mpya ya viwango vya nyuzi joto katika miezi
sita ya kwanza.
Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani
(WMO), ambalo limesema barafu ya bahari ya Arctic iliyeyuka mapema na kwa kasi,
ambayo ni ishara nyingine ya mabadiliko ya tabianchi.
Aidha shirika hilo limesema kuwa viwango vya gesi ya
mkaa, ambavyo vinachangia ongezeko la joto duniani, vilifikia upeo mpya.
Katibu
Mkuu wa WMO Petteri Taalas amesema kuwa, hali ya El Nino ya 2015/2016
imechangia viwango hivi vya joto.
0 comments:
Post a Comment