Tuesday 12 July 2016

HII NDIO NCHI INAYOONGOZA KWA WATU WAKE KUWA NA HIV..!

Marekani imeiahidi Afrika Kusini msaada wa dola milioni 410, katika vita dhidi ya ugonjwa wa
Ukimwi.
Afrika Kusini ina idadi kubwa zaidi ya watu wanaoishi na virusi vya HIV duniani.
Msaada huo wa Marekani utasaidia katika kutanua mpango wa kutoa dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo kwa waathiriwa zaidi ya milioni tatu.
Watu milioni 6.8 nchini humo wameathirika na Ukimwi.
Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na HIV na Ukimwi UN AIDS, watu laki 1 na elfu 80 walikufa Afrika Kusini mwaka jana kutokana na ugonjwa huo.

Wiki ijayo Afrika Kusini itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na UN AIDS, wa kujadili lengo la malengo ya maendeleo endelevu la kukomesha janga la Ukimwi ifikapo mwaka 2030.

0 comments:

Post a Comment