Jaji Mkuu wa tanzania Mohamed
Chande amesema kuwa, jopo la majaji linatarajiwa kuingia darasani ili
kujifunza sheria mpya ya kuendesha kesi za ufisadi.
Kesi
hizo zitakuwa zinaendeshwa katika Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi, na
tayari majaji 14 wa wataanza kozi maalumu ya siku tano katika Chuo cha Sheria
kilichopo Lushoto, Tanga.
Amesema hatua hiyo
inakuja baada ya wiki iliyopita, Bunge kupitisha sheria ya uhujumu uchumi ya
mwaka 2002 ikiwa na maboresho mbalimbali.
Ameongeza kuwa maeneo yapo
tayari na wameshapeleka wasajili na watendaji ambao wameanza kufanya kazi,na baada
ya michakato mingine kukamilika kila kitu kitakuwa sawa na majaji wataanza kazi.
0 comments:
Post a Comment