Ripoti mpya
inasema watoto wanaonyonya vidole au kung'ata kucha zao kwa meno huenda
wasipate
matatizo ya kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula
fulani.
Kwa mujibu wa waandishi katika jarida la Pediatrics huo ni ni
usafi dhanio,kwani yatokanayo na baadhi ya wadudu huimarisha mfumo wa kinga ya
mwili.
Unyonyaji wa kidole gumba na ung’ataji wa kucha umeonekana
kuzuia baadhi ya alergy.
Kati ya watu elfu moja wenye umri wa kati ya miaka mitano
hadi thelathini na mbili,walifanyiwa uchunguzi kwa muda nchini New Zealand.
Lakini tabia hii ya unyonyaji vidole na ung’ataji kucha
haisaidii watu wenye pumu au mtu anapopata homa kali.
Uchunguzi uliofanywa na kurekodiwa kwa watoto wenye umri wa
kati ya miaka mitano na kumi na moja na wengine waliofanyiwa vipimo ni wenye
umri kati ya miaka kumi na tatu na thelathini na miwili.
Huku thuluthi moja ya watoto hao ni wanyonyaji wa vidole mara
kwa mara au hung’ata kucha zao na katika vipimo walivyofanyiwa watoto hao
wameonekana kuwa wana kiwango kidogo cha kuathirika kutokana na mazingira hewa
au kula vyakula fulani.
0 comments:
Post a Comment