Mamia
ya watu watavua nguo zao na kupigwa picha wakiwa tupu kusherehekea utamaduni
katika mji wa Hull, Uingereza.
Tukio hilo litakuwa la
kusherehekea mji huo kama Mji wa Utamaduni.
Washiriki watapakwa rangi ya
samawati Jumamosi na kisha wapigwe picha wakiwa katika maeneo mashuhuri jijini
humo kama sehemu ya mradi uliopewa jina Sea of Hull.
Mradi huo unatekelezwa na mpiga
picha Spencer Tunick na unadhaminiwa na taasisi ya Sanaa ya Ferens Art Gallery.
Picha zitakazopigwa zitawekwa na
kuoneshwa kwa umma wakati wa tamasha ya sanaa ya 2017 itakayoendelea kwa mwaka
mmoja.
Tunick, anayetoka New York,
amewahi kufanya kazi kama hiyo kwingine.
Amewahi kupiga picha za watu
wengi wakiwa uchi Sydney Opera House, Place des Arts mjini Montreal, Mexico
City na mjini Munich nchini Ujerumani Germany.
Bw Tunick amesema kazi zake
“hugusia historia ndefu ya Sanaa ya utupu”.
"Mavazi ni Sanaa ya mtu
mwingine,” anasema.
“Fashoni ni Sanaa. Kwa kuondoa
hilo (mavazi), nitakuwa nafanya kazi na usawa na maumbile katika umaridadi
wake.”
Watu karibu 2,000 wamejiandikisha kupigwa picha tangu
wazo hilo litangazwe mwezi Machi.
Baraza la mji wa Hull limesema
baadhi ya barabara zitafungwa wakati wa shughuli hiyo Jumamosi asubuhi.
0 comments:
Post a Comment