Waziri
mkuu Kassim Majaliwa, amepiga marufuku uvutaji wa shisha nchini, na kulitaka
Jeshi la
Polisi kufuatilia na kutokomeza matumizi ya sigara hiyo ili kuokoa
makundi ya vijana ambao wanajihusisha na ulevi huo.
Waziri mkuu Majaliwa alitoa agizo hilo juzi jijini Dar
es Salaam katika futari iliyoandaliwa na waumini wa dini ya kiislamu wa
madhehebu ya Shia.
Amesema shisha inamchanganyiko mwingi na wanaweza
kutia maji, lakini wakati mwingine maji hayo yakawa yamewekwa gongo na vilevi
vingine mbalimbali.
Waziri mkuu Majaliwa alisema mtu anapotumia kilevi
hicho anakuwa anashawishika kila siku kukitumia, na kwamba pale anapokikosa
husikia mwili unasisimka na hivyo kulazimika kuifuata popote pale ilipo.
Juzi akizungumza jijini Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa huo
Paul Makonda, alipiga marufuku uvutaji wa sigara hadharani, pamoja na matumizi
ya sigara ya shisha mkoani humo kwa kuwa inachanganywa na vilevi vinavyoharibu
vijana.
Alisema utafiti alioufanya chini ya Mamlaka ya Chakula
na Dawa Tanzania (TFDA), shisha ina madhara makubwa kwa wanaoivuta na wasiovuta
kwa kusababisha saratani ya mapafu na koo.
Msikie hapa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda,akizieleza adhari anazoweza kuzipata mtumiaji wa shisha.
0 comments:
Post a Comment