Utafiti wa
mmoja kiafya duniani umeonyesha ongezeko la asilimia 82 la watu wanene kupita
kiasi kati ya mwaka wa 1990 na 2010, likasema jarida la tiba la Uingereza, ‘The Lancet’, Volume 387, la
Aprili 2, 2016
Vifo vinavyotokana na kunenepa
kupita kiasi ni mara tatu zaidi ya vifo vinavyosababishwa na kukosa chakula
chenye lishe, ingawa bado nchi nyingi zinapambana na ukosefu wa chakula.
Majid Ezzati, ambaye ni Profesa wa
Afya ya Mazingira Duniani katika chuo cha Imperial cha London, Uingereza,
alikuwa ni mmoja wa watafiti hao.
Ezzati alisema: “Katika ulimwengu
ambao miaka 20 iliyopita haukuwa na chakula cha kutosha, sasa hivi tunapata
magonjwa yanayotokana na kula kupita kiasi na vyakula vinavyoleta madhara, hata
katika nchi zinazositawi.”
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa
na Utafiti wa Kitaifa wa Afya na Lishe nchini Marekani (NHANES), uchunguzi wa
hivi karibuni unaonyesha kuwa asilimia 40 ya wanawake wa Marekani ni wanene
kupita kiasi, asilimia ambayo ni kubwa zaidi katika historia ya dunia. Takwimu
hizo zinaonyesha kuwa wanaume wanene kupita kiasi nchini humo ni asilimia 35.
0 comments:
Post a Comment