Kamati iliyoundwa
kuchunguza utaratibu uliotumika kumhamisha Faru John kutoka hifadhi ya
Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyopo kwenye Hifadhi ya
Grumeti Serengeti, imependekeza hatua za kinidhamu dhidi ya maofisa wawili wa
Serikali waliohusika na uahamishwaji wa mnyama huyo.
Kamati haikufafanua
aina ya hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kwa maofisa hao, lakini imependekeza
hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.
Aidha, Kamati hiyo
imegundua kuwa Faru John alikufa kifo cha asili ambacho kilisababishwa na
kutokupatiwa huduma za msingi za matibabu, ambapo imependekeza hatua za
kinidhamu zichukuliwe kwa wahusika kwa sababu hakukuwa na kibali rasmi cha
kumhamisha kwenda mazingira ambayo yalisababisha kifo chake.
Kwa upande wake,
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel
Manyele alitoa mapendekezo hayo wakati akikabidhi ripoti hiyo kwa Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa juu ya uchunguzi walioufanya kuhusu uhamishwaji na kifo cha mnyama
huyo.
Hata hivyo, Kamati
hiyo imependekeza hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya Mkurugenzi wa
Wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Profesa Alexander
Songorwa na Daktari wa Shirika la Hifadhi la Taifa (Tanapa), Dkt. Moris Kileo.
0 comments:
Post a Comment